WIZARA NA WADAU WA MICHEZO WAMPA TANO RAIS SAMIA
Na. John Mapepele Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo nchini leo Machi 29, 2022, wanaadhimisha kilele cha wiki ya Rais Samia ikiwa ni kampeni maalum ya kuelimisha umma, kujadili na kutafakari mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye mwaka mmoja wa utendaji wake tangu aingie madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Machi 19, mwaka jana. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ndiye Mgeni Rasmi atakayeongoza kongamano hilo la michezo katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Michezo. Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Benjamini Mkapa kuanzia saa nane mchana na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo nchini. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo. Yusuph Singo Omary, wadau mbalimbali wa michezo ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sa...

Comments
Post a Comment