Posts

Waziri Mchengerwa azindua zoezi la kitaifa la kusaka na kuibua vipaji "mtaa Kwa mtaa."

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni,  Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Oktoba 16, 2022 amezindua  zoezi la  kitaifa la  kuibua na kusaka vipaji  vya Sanaa la "Mtaa kwa Mtaa" eneo la  Ikwiriri wilayani Rufiji, zoezi ambalo litafanyika nchi nzima. Akizindua zoezi hilo katika eneo la Ikwiriri, Mhe. Mchengerwa amesema eneo linalofuata baada ya uzinduzi wa leo ni Mkoa wa Arusha ambapo litafanyika kila mtaa ili kuibua vipaji kwenye sanaa. Amewataka watanzania  wenye vipaji vya Sanaa kujitokeza wakati wa zoezi hilo likiendelea  ili waweze kuendelezwa baada ya kuibuliwa, huku akisisitiza  kauli ya Kipaji chako ndiyo mtaji wako. "Ndugu zangu hii ni ndoto ya Mheshimiwa Rais wetu, Rais anatamani kuona misingi iliyowekwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere ya kuthamini na kuendeleza Sanaa inaendelezwa ili kuwanufaisha vijana" amesisitiza,  Mhe. Mchengerwa   Amezitaka mamlaka za wilaya na mikoa kote nchini kusai...

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo yashirikiana na Wizara ya Maliasili kuitangaza Tanzania, kukuza utalii.

MCHENGERWA AITAKA COSOTA KUTOA ELIMU YA KANUNI MPYA ZA ADA ZA VIBEBEA KAZI ZA SANAA NA MAKAMPUNI YA WASANII

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameitaka Taasisi ya Hakimiliki nchini (COSOTA)  kutoa elimu ya kutosha kwa wadau hususan wabunge      kuhusu mabadiliko makubwa yanayofanywa na taasisi hiyo ya kimuundo na kisekta ili kusaidia kuinua maisha ya wadau wa sekta ya Sanaa nchini. Waziri Mchengerwa ameyasema haya leo Septemba 14, mara baada ya kupitishwa  yeye na Naibu wake Mhe, Pauline Gekul na Menejimenti ya taasisi hiyo kwenye kikao cha kujadili  rasimu ya kanuni ya uanzishwaji wa Ada kwa vibebea kazi za ubunifu (blank device) na uanzishwaji wa makampuni binafsi ya   wasanii ya ukusanyaji na ugawaji mirahaba (CMO). Amewataka kuharakisha mchakato wa kukamilisha rasimu hizo ili  zisainiwe  na kuanza kutumika mara moja hatimaye wasani na wadau mbalimbali wa kazi za Sanaa waweze kunufaika na kazi zao. "Harakisheni, ninakwenda kuisaini kanuni hizi mara moja ili wasanii  wafaidi matunda ya...

Mhe.Mchengerwa ampokea Rais wa FIFA

Image
  Na John Mapepele, Arusha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa usiku huu ameongoza ujumbe wa kumpokea Rais wa FIFA Gianni Infantino anayekuja kuhudhuria mkutano wa 44 wa Shirikisho la  Soka Barani Afrika (CAF). Mkutano huo wa kwanza wa kihistoria unafanyika kwa mara ya kwanza nchini huku zaidi ya nchi 58 kutoka sehemu mbalimbali duniani zikishiriki. Mhe. Mchengerwa amemkaribisha  Rais wa FIFA Gianni na kumpatia salamu za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumwelezea  jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ambapo Rais wa FIFA ameelezwa kuridhishwa na maendeleo ya Michezo. Amepongeza kazi kubwa huku akisema amefurahishwa na makaribisho hayo. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu mia tano na kuangaliwa na watu zaidi ya bilioni moja. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kassim Majaliwa anatarajiwa kumwakilisha Mhe. Rais. Katika mkutano huo CAF inakwenda kuzindua  mashindano maalum ya soka y...

Waziri Mchengerwa akutana na UNESCO, aunda tume ya uanzishwaji wa chuo Kikuu cha Kiswahili

Image
  Na John Mapepele,  Waziri wa Utamaduni, Sanaa Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amekutana  na ujumbe wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na ameunda tume kwa ajili ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Kiswahili nchini ikiwa ni mkakati kabambe wa kubidhaisha lugha ya Kiswahili  katika  mabara yote duniani. Mhe, Mchengerwa ameunda tume maalum ya uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Kiswahili kufuatia  ombi lake alilolitoa  kwa  shirika  la UNESCO wakati wa siku ya  maadhimisho ya Kiswahili duniani   mwaka huu iliyofanyika  kwa mara ya  kwanza  Julai 7, 2022.  Akizungumza mara baada ya mkutano na ujumbe wa UNESCO ofisi za Tanzania leo Agosti 5, 2022 ofisini kwake jijini Dar es Salaam amesema matajio ya  Serikali ni kuona kuwa Kiswahili kinavuka mipaka  ya   Tanzania. Aidha, Mhe Mchengerwa ameipa tume  hiyo siku  tano  kukamilisha andiko  hilo ili liwasi...

Mhe. Mchengerwa amwaga vifaa vya michezo shule zote wilaya ya Rufiji, aanzisha ligi ya Sensa

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Rufiji.  Mhe, Mohamed Omary Mchengerwa ametoa vifaa vya michezo kwa shule zote za msingi na Sekondari na wanafunzi wanamichezo wote  wanaoshiriki kwenye mashindano ya michezo kwa shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Mashindano  ya Shule za Sekondari (UMISSETA) kwa mwaka 2022 Wilaya ya Rufiji. Mhe. Mchengerwa amekabidhi  vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Julai 17, 2022 kwenye  shule ya Sekondari ya Ikwiriri   Wilaya ya Rufiji ambapo amesema ameamua  kufadhili vifaa hivyo katika Wilaya ya Rufiji ili kuiendeleza michezo kwa kuwa michezo ni biashara  na ajira kubwa  kwa vijana. “Nimeamua kusaidia vifaa hivi kwakuwa natambua  kwa sasa michezo ni miongoni mwa chanzo cha ajira na biashara kubwa duniani hivyo ni vema kufanya michezo kwa umakini mkubwa ili kujipatia ajira” amefafanua Amewataka wachezaji hao kuwa na nidhamu na kujituma kwa kufanya mazoezi i...

Tuliahidi, tumetekeleza: Tanzania Yaiongoza Dunia MASIKIDU

Image
  Tanzania leo imeiongoza dunia kuadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani (MASIKIDU) kwa matukio mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali duniani yakiongozwa na hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi uliopewa jina la mmoja wa waasisi wa lugha hiyo, Ukumbi wa Kimtaifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.  Jijini Dar es Salaam na Dakar: Akiongoza hafla hiyo Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Phillip Mpango, alipokea salaam za Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliyeko Dakar Senegal kwa kikao cha AU. Maputo, Msumbiji: salaam kutoka kwa Rais Phillep Nyusi wa Msumbuji nazo zilipambanhadla ya Dar es salaam. Bujumbura, Burundi: Rais Ndaishimana wa Burundi naye pia aliwasilisha salaam zake kwa Kiswahili akiwatakia kheri Watanzania wenye Kiswahili chao. Beijing: Nchini China mjadala mzuri wa Kiswahili uliohusisha wataalamu mbalimbali wa Kichina wanaozungumza Kiswahili umefanyika ukiratibiwa na Ubalozi. New Yotk. Jijini NY, Marekani, kwenye makao makuu ya UN, Ubalozi wa Tanzania umez...