Posts

Showing posts from August, 2022

Mhe.Mchengerwa ampokea Rais wa FIFA

Image
  Na John Mapepele, Arusha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa usiku huu ameongoza ujumbe wa kumpokea Rais wa FIFA Gianni Infantino anayekuja kuhudhuria mkutano wa 44 wa Shirikisho la  Soka Barani Afrika (CAF). Mkutano huo wa kwanza wa kihistoria unafanyika kwa mara ya kwanza nchini huku zaidi ya nchi 58 kutoka sehemu mbalimbali duniani zikishiriki. Mhe. Mchengerwa amemkaribisha  Rais wa FIFA Gianni na kumpatia salamu za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumwelezea  jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ambapo Rais wa FIFA ameelezwa kuridhishwa na maendeleo ya Michezo. Amepongeza kazi kubwa huku akisema amefurahishwa na makaribisho hayo. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu mia tano na kuangaliwa na watu zaidi ya bilioni moja. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kassim Majaliwa anatarajiwa kumwakilisha Mhe. Rais. Katika mkutano huo CAF inakwenda kuzindua  mashindano maalum ya soka y...

Waziri Mchengerwa akutana na UNESCO, aunda tume ya uanzishwaji wa chuo Kikuu cha Kiswahili

Image
  Na John Mapepele,  Waziri wa Utamaduni, Sanaa Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amekutana  na ujumbe wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na ameunda tume kwa ajili ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Kiswahili nchini ikiwa ni mkakati kabambe wa kubidhaisha lugha ya Kiswahili  katika  mabara yote duniani. Mhe, Mchengerwa ameunda tume maalum ya uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Kiswahili kufuatia  ombi lake alilolitoa  kwa  shirika  la UNESCO wakati wa siku ya  maadhimisho ya Kiswahili duniani   mwaka huu iliyofanyika  kwa mara ya  kwanza  Julai 7, 2022.  Akizungumza mara baada ya mkutano na ujumbe wa UNESCO ofisi za Tanzania leo Agosti 5, 2022 ofisini kwake jijini Dar es Salaam amesema matajio ya  Serikali ni kuona kuwa Kiswahili kinavuka mipaka  ya   Tanzania. Aidha, Mhe Mchengerwa ameipa tume  hiyo siku  tano  kukamilisha andiko  hilo ili liwasi...